GET /api/v0.1/hansard/entries/1476033/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1476033,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476033/?format=api",
    "text_counter": 422,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia suala la ugavi wa pesa zitakazokwenda katika serikali za kaunti 47 katika nchi yetu ya Kenya. Jambo la kusikitisha ni kwamba hapo awali, tulikuwa tumekubali kwamba kiwango tulichokuwa tumeweka cha shilingi bilioni 415 kingetosha vizuri. Bw. Spika wa Muda, sisi tukakubaliana ya kwamba irejeshwe chini mpaka ifike shilingi bilioni 400. Limekuwa ni jambo la kusikitisha kuona ya kwamba kuna marekebisho zaidi ya kurudisha chini mpaka shilingi bilioni 350. Nguzo za uchumi wa nchi yetu ya Kenya zinategemea serikali zetu za ugatuzi. Kwa sababu katika miaka mingi, tumekuwa katika Serikali ya Kitaifa na maendeleo yake yamekuwa nadra sana. Ninakumbuka katika Kaunti ya Kilifi, ilikuwa na ambulensi moja na ilikuwa inaharibika saa zote. Watu walikuwa hawawezi kupata maslahi yao ya kubebwa na ambulensi wanapokuwa wagonjwa. Sasa kuna ambulensi zaidi ya kama saba katika Kaunti ya Kilifi. Hivyo ni kumaanisha, serikali ya ugatuzi inafanya kazi yake vilivyo. Bw. Spika wa Muda, tunakataa Mswada huu kwa sababu umetengenezwa kurejesha pesa chini ili serikali zetu za ugatuzi ziingie katika shida ya kufanya kazi ambayo wanatakikana kufanya. Inakuwa shida kubwa sana kwa gavana kujipanga. Ikiwa hapo awali alikuwa amejipanga kufanya jambo fulani na hivi sasa tunamwambia ya kwamba pesa hizo haziji mashinani, atafanya nini? Seneti hii ndiyo Bunge ambalo linahusika na serikali za ugatuzi. Sisi ni kama wale watu wamevaa kiatu. Avaae kiatu, akisikia kina maumivu ama kinamuumiza, anajua pale ambapo kinaumiza. Sisi maseneta ndiyo tunajua ugonjwa wa kaunti uko wapi. Na kunazo sababu za kusema ni kwa nini kaunti zitenge pesa za maendeleo ya mahosipitali, madawa, The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}