GET /api/v0.1/hansard/entries/1476034/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1476034,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476034/?format=api",
    "text_counter": 423,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "barabara, shule za chekechea na maendeleo kadha wa kadha wanayotakikana waendelee nayo. Ni sisi tunaoelewa shida ambayo zinakuba serikali za ugatuzi na kazi zetu tulizonazo hapa. Ikiwa nitakupa taarifa, niruhusu niseme kwamba Kipengele cha 96, sheria ya kwanza, inasema kuwa kazi kubwa ya Seneta ni kuwakilisha kaunti na pia kuleta mahitaji ya kaunti ya ugatuzi na kulinda maslahi hayo. Hii ni kazi ambayo inahitaji uangalifu na udhalilifu wa hali ya juu sana kuona ya kwamba mahitaji haya yameweza kupatikana. Lakini cha muhimu zaidi kulingana na Mswada huu ambao upo mbele yetu, ni Kipengele cha 96(5) ambacho kinaongea juu ya taratibu za Seneti katika kazi zake Seneti inaweza kujadili na kusaidia kuona ya kwamba imeongeza zile pesa ambazo zinatakikana kutoka katika kitita cha hazina ya Serikali kuu na kinachopelekwa katika serikali za ugatuzi. Natuhakikishe pesa ambazo zinagawanywa, kila kaunti ipate haki yake na pesa hizo zitumiwe vyema. Hivi leo, tunaambiwa tupunguze pesa hizi mpaka zifike shilingi bilioni 350. Mimi nimekuwa ndani ya Bunge hili tokea lianze. Ninasema kuwa kama taratibu ya Seneta ambaye anajua historia ya Seneti hii. Kitu cha kwanza unachostahili kufanya ukitaka hawa maseneta wote waende nyumbani ni kupinga kuongezwa kwa pesa zitakazokwenda katika serikali za mashinani. Bw. Naibu Spika, hili ni onyo kubwa sana kwa sababu ukiangalia wote huweza kupoteza hiyo nafasi kwa sababu ya kitu kimoja tu, umekukosa kupeleka pesa nyumbani. Hivi sasa, kila Seneta hapa anajukumu lake la kuweza kuchukua nafasi hiyo kuonekana ya kwamba yeye amefanya bidii ndani ya Seneti na amepeleka hizo pesa nyumbani."
}