GET /api/v0.1/hansard/entries/1476056/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1476056,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476056/?format=api",
"text_counter": 445,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Pesa zinacheleweshwa kutoka kwa Serikali kuu kwenda kwa serikali za kaunti. Hata zile wanatarajia baada ya kupitishwa kwa disbursement schedule, vilevile haziwezi kufika kwa wakati. Kwa hivyo, haiwezekani kwamba fedha za serikali za kaunti zipunguzwe wakati serikali kuu ina uwezo wa kukopa na kukusanya fedha zaidi ya zile zinazohitajika kukusanywa kwa ule mwaka unaofuata. Bw. Spika wa Muda, jambo la tatu ni kwamba tunapozungumzia asilimia ya fedha zinazoenda kwa kaunti, tunatumia hesabu za miaka minne nyuma. Kwa sasa, tunatumia mwaka wa 2020/2021 kugawa fedha zilizokusanywa mwaka huu wa 2024/2025. Hiyo inatoa taswira mbaya kwa sababu fedha ambazo tunazungumzia ni zile zitakusanywa mwaka huu, sio zile zilizokusanywa miaka minne iliyopita."
}