GET /api/v0.1/hansard/entries/1476060/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1476060,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476060/?format=api",
    "text_counter": 449,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Tukiangalia pia sheria ya National Social Security Fund (NSSF), pia inaongeza gharama kwa sababu, tajiri na pia mfanyakazi wanalipa. Kwa hivyo, itabidi serikali za kaunti ziingie mifukoni zaidi ili walipie hizo tofauti zinazotakiwa kulipwa kwa wafanyakazi wao. Tukiangali masuala ya wafanyakazi wa afya ya umma, Community Health Promoters (CHPs), ni jambo ambalo serikali imetilia mkazo. Kwamba, kaunti zetu ziajiri hawa watu ili wapate ajira na wasimamie hii sheria mpya ya afya. Kwa hivyo, hii pia ni gharama inayo ongezeka bali na ile nyongeza ya mishahara ambayo iko katika makubaliano kati ya vyama vya wafanyakazi wa kaunti na serikali za kaunti. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}