GET /api/v0.1/hansard/entries/1476066/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1476066,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476066/?format=api",
    "text_counter": 455,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Jambo la msingi ni kwamba pesa nyingi zinatumika katika mambo ambayo hayaleti maendeleo katika kaunti zetu. Pesa nyingi zinatumika katika safari ambazo hazileti wateja. Pesa nyingi zinaenda kwa mikutano ambayo haileti maendeleo katika kaunti zetu. Kwa hivyo, kuna haja ya kaunti zetu kupunguza matumizi ambayo siyo muhimu. Tumeambiwa katika muongozo wa serikalini kwamba kutakuwa na ukazaji wa mishipi lakini tunaona bado kuna matumizi ambayo hayana msingi wowote kisheria. Kwa hivyo, kaunti zinadorora kihuduma."
}