GET /api/v0.1/hansard/entries/1476074/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1476074,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476074/?format=api",
"text_counter": 463,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Kwa mfano, utapata katika kaunti nyingi, hospitali au zahanati, hazina madawa. Madaktari wanachelewa kulipwa mishahara yao. Wale CHPs ambao wameajiriwa ili wasaidie kupeleka huduma za afya mashinani hawalipwi mishahara yao kwa wakati unaofaa. Hii inamaanisha kwamba huduma zinadorora katika kaunti zetu. Hakuna soko mpya ama ECDE ambazo zinajengwa. Haya yote yanatuonyesha kwamba ugatuzi unapungua kasi kuliko ulivyotarajiwa kukuwa kutoka mwaka wa 2013 mpaka 2022. Kupunguza hizi fedha ambazo zitatarajiwa kuja kwa kaunti zetu zitachangia pakubwa kudorora zaidi kwa huduma katika kaunti zile. Tumezungumzia masuala ya MES. Mradi huu ulikuwa mzuri. Lakini vile vifaa vyote ambavyo vilinunuliwa vinakaribia kufika ukingoni na haviwezi kutoa huduma baada ya miaka kumi kutoka mradi huu uzinduliwe. Hivyo basi, kuna haja ya kubadilisha vifaa vipya. Kwa mfano, sehemu ambazo mashine za dialysis zilikuwa zinatumika zinafaa kupewa mashine mpya kwa sababu miaka kumi inaenda kuisha. Pia zile software zinazotumika katika mashine hizo zimebadilika kutokana na mambo mapya kuingia katika mitindo ya kuziendesha. Wanafaa kuwekeza kwenye mashine mpya ili ziendelee kutoa huduma kwa wananchi katika sehemu zile. Iwapo hizi fedha zitapunguzwa ina maana kwamba miradi yote ambayo inatarajiwa kufanywa na kaunti zile itakoma. Hivyo basi, wananchi watakosa huduma muhimu katika kaunti zetu. Serikali ilisema kwamba itapunguza ubadhirifu. Hata hivyo, tabia hiyo bado ipo. Bado kuna safari za nje kwa Mawaziri na ofisi zingine kubwa za Serikali. Fedha zinapotea kiholela katika mashirika na Wizara ambazo the Ethics and Anti-Corruption Commission (EACC) inachukua muda kuwapeleka mahakamani wanaohusika katika ubadhirifu wa fedha. Sio sawa kupunguza fedha ambazo zitapelikwa katika kaunti zetu. Lazima Serikali ijifunge kibwebwe na kuhakikisha kwamba inakusanya shilingi trilioni 2.6 kama ilivyonuia. Wahakikishe kwamba hakuna fedha zinazopangwa kwenda katika kaunti zetu zinapunguzwa. Wakati Wanakamati walipokuwa wanachunguza Mswada huu, tulipata maoni kutoka mashirika mengi ikiwemo Baraza la Magavana, yani CoG. Wengi walikataa kupunguzwa kwa fedha hizo kwa sababu inamaanisha kwamba huduma katika kaunti zetu zitadorora. Bw. Spika wa Muda, napinga Mswada huu wa kurekebisha the DORA. Vilevile, wamesema kwamba Bunge lina uwezo wa kubadilisha the DORA. Hatukatai kwamba sheria zinazopitishwa zinaweza kubadilishwa na Bunge hili na Bunge la Taifa. Iwapo kaunti zetu zitafanya mipango yao ya mwaka na bajeti kusomwa na kupitishwa, haitakuwa vizuri Mswada wa kupunguza fedha zitakazokwenda katika kaunti zetu kuletwa katikati ya mwaka. Iwapo kuna marekebisho yoyote, yanafaa kufanywa kabla ya the DORA pamoja na the County Allocation of Revenue Act (CARA) kupitishwa katika Seneti."
}