GET /api/v0.1/hansard/entries/1476132/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1476132,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476132/?format=api",
    "text_counter": 45,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika, kwa kunipa fursa hii. Natoa shukrani zangu na kongole kwa dada yetu kutoka Pwani, Bi. Akida, ambaye ameweza kufika kiwango cha kimataifa. Hii ni kuonyesha kwamba talanta za soka ziko kila mahali, hata kule Pwani. Mwezi uliopita, tulipeleka kijana kutoka Pwani kwenye kambi ya mbio kule Bomet. Kwa hivyo, tunakosa tu vifaa na mafunzo, lakini dada yetu ametuonyesha kwamba Wapwani tunaweza kusaidia kusukuma gurudumu la talanta mpaka kufika kwenya ngazi za kimaitafa, tukijua kwamba talanta ni ajira. Ahsante, Mhe. Spika. Kongole dada yetu, Akida."
}