GET /api/v0.1/hansard/entries/1476239/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1476239,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476239/?format=api",
"text_counter": 152,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana Mhe. Spika. Swali langu kwa Waziri ni hili. Tunajua Football Kenya Federation (FKF) watapiga kura zao hivi karibuni. Nakuuliza watawezaje kupiga kura bila kuwa na Kamati ya kushughulikia manung’uniko ( Appeals committee) ? Kwa nini ile bodi ya uchaguzi ipo katika himaya ya wanaowania? Ni kama vile Rais anataka kura, lakini ile komisheni ya kusimamia kura iko ndani ya ikulu. Utakuwaje uchaguzi wa haki? Kisha nauliza, ni kanuni zipi umeweka kuhakikisha kuwa vile vipimo vya FIFA vimefuatwa? La mwisho, huko mashinani, watoto wamekuwa wakicheza mpira, lakini wanachangiwa kama maskini. Watoto wanatoka Mombasa wakitaka kuja Nairobi kwenye mashindano, wanachangiwa mpaka sehemu ya kulala. Inakuwa shida mpaka wanalala kwenye maveranda. Nauliza, kama tunakuza talanta, mbona tusiweke pesa huku chini? Hao watoto wakitoka, watoke na nguvu wakijua tunaelekea sehemu ambayo ni nzuri. Ahsante sana."
}