GET /api/v0.1/hansard/entries/1476325/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1476325,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476325/?format=api",
"text_counter": 238,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Ahsante. Waziri, mwanzo, ningependa kukupongeza na kukushukuru wakati ulikuwa Waziri wa Barabara, Usafiri na Kazi za Umma. Ulijua Lamu Mashariki haina barabara na ukafanya mipango mizuri. Ahsante. Saa hii pia, ningependa ufikirie kuhusu Lamu Mashariki katika upande wa michezo. Hakika kwa miaka kadhaa au tangu uhuru upatikane, hakuna kitu kimefanywa katika Eneo Bunge la Lamu Mashariki katika upande wa michezo. Nimesikia mipango yote ambayo umezungumzia. Kaunti ya Lamu haina uwanja wa Serikali ya Kitaifa wala ya kaunti. Katika mipangilio yote, sisi tunaachwa nyuma. Nakuomba kwa hisani yako kama unaweza kutaja kitu kimoja ambacho kimefanywa Lamu Mashariki na hii Wizara. Niambie tu kimoja. Na kama hakipo, kuanzia sasa, utuweke akilini ili chochote kile kinachofanywa huku, hata nasi tufanyiwe. Ahsante. Umezungumzia mambo ya vilabu ambavyo viko. Labda unaweza kuziwezesha. Kama huzijui, kuna klabu ndogo ambazo zinaweza kuwezeshwa kama vile King Loyal, Biladi, Faaza United na zingine nyingi. Ahsante."
}