GET /api/v0.1/hansard/entries/1476545/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1476545,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476545/?format=api",
    "text_counter": 96,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "walipima tonnes kwa sababu wanakufinya. Kwa sababu hii, wakulima wengi wamekosa ari ya kurudi mashambani kulima. Ndio maana tunasema wakulima wapewe nafasi ya kushughulikia mambo ya factory ya miwa ili waweze kuangalia haki yao. Wakipewa mwanya huu watakaa pamoja na wale wahusika ili waweze kujua haki zao za kimsingi, ukulima na kuhakikisha kuwa upanzi wa miwa unaangaliwa vizuri. Mazao pia yakitoka watapata faida nzuri. Makampuni mengi ya sukari yamefungwa kwa sababu wenyewe hawakuwa na mwongozo mzuri katika zile factory zao. Kulikuwa pia na utepetevu mkubwa sana. Wengi walikuwa wakinyanyasa wakulima, jambo ambalo liliwafanya kurudi nyuma na kuacha kupanda miwa. Kwa sababu hiyo, factory nyingi zilifunga kazi. Mkulima yeyote, si wa miwa tu kwa sababu hata Mombasa tuna wakulima wa korosho, anafaa kusaidiwa na Serikali. Tunaunga mkono jinsi Serikali inasukuma sehemu nyingine katika ukulima, lakini wasiangalie sehemu moja tu. Mimi, kama mama Zamzam, nina support wakulima wa sukari. Pia, ningeomba wakulima wa korosho na nazi waweze kuangaliwa kwa sababu zote zinaleta rasilimali nchini. Kwa upande wa ukulima wa nazi, utapata kwamba zinatolewa kutoka India na China ilhali kuna wakulima ndani ya taifa letu lakini hawashughulikiwi. Ningependa kumshukuru ndugu yangu, Mhe. Nabulindo, kwa kuleta Hoja hii ya kutetea ukulima wa sukari. Pia, tunafaa tujue kuwa hawa wenye factory wanatengeneza pesa nzuri sana. Wanafaa kutoa mafunzo kwa hawa wakulima ili waweze kuwasaidia na kushirikiana nao kwa ukaribu. Hii ni muhimu kwa sababu mkulima ataelewa kuwa akitoa mazao yake, hakika atajua kile anachostahili kupata. Hii itahakikisha kuwa anapata moyo wa kuzidi kulima miwa. Ninamuunga mkono ndugu yangu. Kuna Mswada ambao utakuja hapa. Singependa kuujadili wakati huu, lakini Kenya iko katika hali ngumu sana. Tunafaa kuangalia sehemu ambazo zinazalisha. Masuala ya kufinya mkulima kuhusu leseni ya hii na ile si vyema. Wakulima kule chini wanapambana na mbolea na mambo mengi. Wakubaliwe kupanda mimea bila kudaiwa leseni ili tuweze kuzalisha. Uchumi ukishashika vizuri, basi tutazungumzia masuala ya kugusa huku na kule. Lakini kwa sasa, wakulima wako chini, na wanastahili kupewa boost na Serikali. Masuala yao yanastahili kuangaziwa kwa sababu hao ndio wanalisha hili taifa. Hivi, tutaweza kuzuia ile sukari inatoka Brazil ambapo kuna nyingine ilikuja na sumu. Tutaweza kuzuia mambo kama haya ikiwa tutampatia mkulima nguvu ya kulima, aone mazao yake na apate kufaidika. Ninaunga mkono Hoja hii, Mhe. Spika wa Muda. Asante."
}