GET /api/v0.1/hansard/entries/1476594/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1476594,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476594/?format=api",
"text_counter": 145,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa Kaunti, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Ninaangalia mjadala ambao umeletwa na dada yangu, Mhe. Esther Passaris, kuhusu karo kuondolewa katika NG-CDF. Wakati nikisoma—na nimetoka katika familia maskini sana—tulikua tunasikia kuna basari ya kitaifa, lakini mtoto wa maskini hangeweza kuifikia. Nilizunguka kila mahali kutafuta ufadhili kusoma. Ndio maana siku zote nitamshukuru marehemu Yusuf Haji, ambaye aliingilia kati akaweza kunisomesha mpaka nikamaliza. Saa hii basari imeingia mpaka kule mashinani. Mtoto wa mashinani anaweza kuipata, akasoma na akamaliza shule. Kuna tu kitu hakina mpangilio. Sasa hata kuna ufadhili wa wanafunzi shuleni na utapata walimu wanasema hakuna kitu kimefika. Kuna sehemu ya karo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}