GET /api/v0.1/hansard/entries/1476595/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1476595,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476595/?format=api",
    "text_counter": 146,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa Kaunti, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "ambayo inalipwa na Serikali, lakini unapata watoto wanafukuzwa shule kwa sababu Serikali haijalipa. Afadhali pesa zote ziende sehemu moja, tujue watoto wangapi wanahesabiwa shule, na wote walipiwe karo. Kama ni Mbunge atalipa, alipe watoto wamalize karo ya shule. Lakini tukiacha huku juu, watu watafanya ufisadi, na zitarambwa kama vile pesa zingine zinavyorambwa hapa Kenya. Hizi pesa hazitafika kule, na wala shule hazitaendelea vizuri. Afadhali tujue Mbunge amepewa pesa aweze kusaidia shule ili watoto wote wawe darasani. Hiyo ni bora kuliko kuacha hizi pesa huku juu, tukisema walimu watanunua vitabu na madawati. Mpaka sasa, watoto wanafukuzwa waende wakanunue dawati. Ndani ya Kenya, mwanafunzi anaenda darasani asome, lakini anatumwa nyumbani aende akanunue dawati. Hizi pesa tukiziacha huku juu, ufisadi utafanywa, na watoto hawatakua darasani. Utapata walimu wameenda nyumbani kwa sababu itakua haina mwelekeo. Lakini wakipewa hawa Wabunge, hizi pesa zitakoma kuwa za Rais na zingine za gavana. Katika Mombasa, Gavana wetu alipewa Ksh600 milioni ya basari. Mimi kama Mama Zamzam nimewahesabu watoto 44,000. Gavana angewalipia wanafunzi hao karo, akiunganisha na pesa za Mbunge, watoto wangesoma bure. Kwa hivyo, mimi ninaona afadhali hizi pesa ziwekwe katika sehemu moja na Rais afanye maendeleo mengine ya taifa. Kuna mambo mengi ambayo yamemzunguka. Gavana ana miundo msingi anafaa kutekeleza kule. Yeye ni rais wa jimbo. Pesa ya basari itoke kwa Gavana na iende kwa Wabunge, na Mbunge ahakikishe kila mwanafunzi yuko darasani na anasoma. Pale ndio Mbunge ataambiwa anapigiwa kura atoke kwa sababu hakufanya hivyo, na watoto hawajasoma. Hauwezi kujua vile hii basari inayozunguka kila mahali inavyotumika. Lakini kuitoa kabisa itafanya shule nyingi kukosa mwelekeo. Tutarudi kama shule zile za zamani. Sisi tulikua tunaenda mpaka na samadi ya ng’ombe na maji. Sijui kama uliona haya yote. Tulikua tunabeba samadi ya ng’ombe kukandika kuta za shule sisi wenyewe. Kitabu umenunuliwa nyumbani unakata kitabu mara nne. Lakini saa hii ninawapongeza hawa Wabunge, hata kama siko katika ule mfumo vizuri. Mgao wangu ni mdogo, na ninautumia kuwarejesha watoto shuleni. Nimewarejesha watoto 350 shuleni ambao walizaa mapema, na ninawalipia karo yote ya shule. Hakuna mtoto anafukuzwa shuleni. Kwa hivyo, hizi pesa zirudi kwa mikono ya hawa Wabunge, lakini wahakikishe kila mwanafunzi ametoka nyumbani, yuko shuleni na analipiwa karo yote. Hakuna mtoto anakaa nyumbani. Hapo tutakuwa tumefanya vizuri. Tukiacha huku juu, tutachekeleana, na elimu itadorora kama vile wakulima wanavyolia saa hii. Asante sana, Mhe. Spika wa Muda."
}