GET /api/v0.1/hansard/entries/1476615/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1476615,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476615/?format=api",
"text_counter": 166,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Ninasimama kuzungumzia Hoja hii ambayo imeletwa na Mheshimiwa Esther Passaris. Lengo lake ni bora kuhakikisha kwamba watoto wetu wanapata elimu inavyofaa. Lakini, tusipoiangalia Hoja hii kwa makini, tutarudi kule tulikuwa. Kwanza kabisa, ni vizuri tujiulize kwa nini taifa letu limechukua mbinu ya ugatuzi? Taifa letu lilichukua mbinu ya ugatuzi kwa sababu hapo awali, pesa zote zilikuwa zinawekwa pale juu. Ilikuwa changamoto kubwa kuhakikisha kwamba Wakenya wengi kule mashinani wamefikiwa na hizi fedha ili wapate elimu. Miaka ya nyuma kabla ya kupata vitengo vya hizi fedha za NG-CDF, NGAAF na zile ambazo zinapitia katika kaunti zetu 47, hakukuwa na usawa upande wa elimu, haswa nikiangalia sehemu ambazo zimetengwa ama za wachache."
}