GET /api/v0.1/hansard/entries/1476616/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1476616,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476616/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "Tukiangalia mambo haswa ya elimu, maeneo mengi hayakuwa yanapata usawa katika fedha za kielimu. Wale waliokuwepo kabla yetu walisema kwamba hizi fedha zishuke pale chini mashinani katika maeneo bunge. Hii ni kwa sababu Mbunge anajua wanafunzi katika eneo bunge lake na wale ambao wana changamoto ya umaskini, shida na uhaba wa fedha, na atawaleta karibu na watapata zile fedha. Fedha hizi zinapopelekwa katika akaunti ile ya juu ya kitaifa, tunajiuliza watu walioko mashinani watazifikia vipi? Leo hii, Mkenya yeyote anaweza kuja katika Ofisi ya Mbunge na ya kaunti aombe bursary . Fedha hizi zikiwa pale juu, huyu Mkenya maskini atazifikia vipi? Ukiangalia hizi fedha za capitation zinazowekewa kila mwanafunzi, tumepata changamoto ngapi? Tumekuwa na changamoto nyingi ambapo shule nyingi zimekuwa zikikosa hizi fedha na wakipata, zinachelewa, ama zinapata robo ama nusu ya fedha hizo. Pili, kuna fedha za miundo misingi ambazo zinatoka kwa Wizara, lakini ukiniuliza, shule zangu nyingi hazipati fedha hizo. Nimekuwa nikifuatilia. Nimeenda katika Wizara, nimeandika barua kuteta, lakini sipati hizo pesa. Pia, zile fedha zinatolewa kisiasa; iwapo utasikizana na yule Waziri ama uko katika upande wa Serikali utazipata, lakini ukiwa Upinzani, utazungumza, hautasikizwa na hakuna kinachofanyika."
}