GET /api/v0.1/hansard/entries/1476618/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1476618,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476618/?format=api",
"text_counter": 169,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Spika wa Muda, jukumu letu ni kuweka utaratibu unaofaa. Kwa mfano, ikiwa fedha za kaunti zitasimamia college na university, basi pesa za Mjumbe ziangalie shule za upili, na pengine fedha za Mwakilishi wa Wadi katika kaunti ziangalie shule maalum. Tunaweza pia kusema kwamba zile fedha zinaletwa na Kiongozi wa Wanawake zishugulikie shule za watoto ambao hawaoni, walemavu na shule ambazo ni maalum. Hizo ndizo njia. Tunafaa tukae chini tufikirie njia ya kutatua jambo hili, ili mwanafunzi mmoja asipate fedha zote na wengine wengi kukosa. Tukizirejesha pale juu, tutapata shida sana. Itakuwa ombaomba; kila siku unaenda ofisi hiyo. Umpigie Waziri simu, akipenda, utapatiwa fedha hizo. Hatutarudi huko."
}