GET /api/v0.1/hansard/entries/1476642/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1476642,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476642/?format=api",
"text_counter": 193,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa ili nichangie Hoja hii muhimu sana kuhusu elimu. Kwanza, ninampongeza Mhe. Passaris kwa kuileta hapa ili watoto wote wapate elimu ya bure. Lakini, ninataka kukosoa ule mfumo ambao anautaka. Haya mambo yamejaribiwa katika taifa hili; kuwa na mfuko moja katika kila sehemu. Hii imesababisha kuzorota kwa taifa zima. Katika sehemu zingine unaskia wakisema wako nyuma ilhali wengine wako mbele. Hii ni kwa sababu ya mfumo wa zile fedha kuwa katika sehemu moja halafu zinagawanywa vile wanavyotaka wao - kisiasa na kwa njia isio sawa. Ikiwa pesa zitaenda mashinani, kila sehemu itapata nafasi ya mgao huo kufadhili wanaohusika."
}