GET /api/v0.1/hansard/entries/1476647/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1476647,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476647/?format=api",
    "text_counter": 198,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "Hizi fedha, kama zingelikuwepo tangu kubuniwa kwa taifa hili, mambo yangelienda vizuri. Shida hizi zote hazingekuwepo. Hata hatungekuwa na sehemu yoyote ya nchi inayosemekana kuwa nyuma, ilhali wengine wamesonga mbele. Hawangelalamikia ukosefu wa barabara ama ukosefu wa shule. Hii inatokana na mgao wa fedha kupunguzwa kiubaguzi na ndiyo sababu sasa hivi kutolewa kwa stakabadhi kama paspoti kumepelekwa katika sehemu tofauti. Shughuli hiyo ilipokua hapa, ilikua nzito. Kwa hivyo, hizi fedha zinastahili kupelekwa maeneo ya chini. Mahali pema ambako fedha zitaweza kusaidia zaidi ni katika NG-CDF. Mbunge apewe fedha na hata aongezewe mradi kuwe na utaratibu wa shule ambazo ziko katika eneo bunge lake. Halafu asibague watu hata kama ni wapiga kura wa kwingine. Asijali watoto wanatoka wapi bali alipe karo yote ya shule. Na mwingine naye alipe yote kule kwingine. Shida hii The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}