GET /api/v0.1/hansard/entries/1476650/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1476650,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476650/?format=api",
    "text_counter": 201,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "Mhe. Spika wa Muda, kuna fedha Wizara ya Elimu inapewa za kujenga shule lakini hakuna jengo linajengwa kutoka Wizara. Majengo shuleni yamejengwa na hazina ya NG-CDF, na National Government Affirmative Action Fund (NGAAF). NG-CDF ndiyo inayojenga shule lakini si Wizara. Juzi walituahidi watatupatia madarasa mawili kila Mjumbe. Hakuna hata moja ambalo wamejenga. Nimesimama hapa kupinga mapendekezo ambayo yametolewa. Tunataka elimu iwe kwa watoto wote; maskini na matajiri. Hii ni kwa sababu ni haki ya kila mtoto Mkenya kupata elimu. Nimesimama hapa kusema fedha hizo zipelekwe kwa Mjumbe. Fedha zipelekwe mashinani kusudi watoto wasome. Asante sana Mhe. Spika wa Muda."
}