GET /api/v0.1/hansard/entries/1476664/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1476664,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476664/?format=api",
"text_counter": 215,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyali, UDA",
"speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Ningependa kwanza kumpa kongole Mhe. Esther Passaris ila nitapinga Hoja yake inayosema kwamba pesa zote ziwekwe katika mfuko mmoja. Hiyo ni sawia na kusema ugatuzi uharamishwe. Ugatuzi uliletwa ili pesa ziweze kufika mashinani. Njia moja ya kipekee ambayo inaonyesha vizuri masuala ya ugatuzi ni pesa za NG-CDF. Hizi ni pesa ambazo zinaweza kumfikia mwananchi wa kawaida. Nimeona Wabunge wengi wamejadili hili jambo na kusema kuna pesa ambazo zipo pale juu na hazijulikani ni za nini, kwa mfano, pesa za basari za Rais. Hii ni basari ambayo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}