GET /api/v0.1/hansard/entries/1476665/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1476665,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476665/?format=api",
"text_counter": 216,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyali, UDA",
"speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
"speaker": null,
"content": "ni vigumu sana kuweza ku identify watoto watakaofaidika mashinani. Lakini, ukiangalia NG- CDF na vile ambavyo tunafanya kazi, mama wa chini kabisa anaweza kumfikia Mbunge na Mbunge kufika mashinani kusaidia watoto kupata elimu. Kwa mfano ukiangalia kwangu, eneo Bunge la Nyali, Kaunti ya Mombasa, ni dhahiri ukitembea utatambua kuwa mgao wa NG-CDF unafanya kazi. Kuhusu pesa ambazo ziko na magavana, Wabunge wengi wamesema kuwa ni kusikilizana. Gavana anaweza kufidia chuo kikuu na Mbunge achukue high school . Utumizi mzuri wa pesa utafanyika katika njia bora zaidi ambayo inaweza kuwa mfano. Hili tutamkumbuka nalo hayati Rais Mwai Kibaki na yule Mbunge ambaye alileta hii nasaha ya kuhakikisha kuwa pesa zinafika mashinani. Kwa hivyo, anavyopendekeza Mhe. Esther Passaris kuwa pesa zote ziwekwe kwa mfuko mmoja... Zikiwekwa kwa mfuko mmoja zitawafikia vipi watu? Tulipigana ili pesa ziondolewe kwenye mfuko mmoja ili zifike mashinani. Kuna magavana ambao wamekalia pesa. Hawawezi kutoa basari. Tuanze kuzingatia vipi tutafikia hizi pesa ambazo haziwafikii wananchi na zile ambazo zinafanya kazi kama za Wabunge. Tufikirie vipi pesa zitaongezwa ili Wabunge waweze kufikia wananchi kule mashinani. Leo ukienda katika kaunti yoyote na uwaulize mama mboga na watu wa boda boda mara ya mwisho kukutana na gavana wao ni lini, hawawezi kukuambia. Watakuambia kuwa hata ofisi hawawezi kukaribia kwa sababu watafukuzwa kama mbwa. Lakini Mhe. Mbunge akiingia katika hayo maeneo, anafikiwa haraka kwa sababu anaingia mashinani kupitia vichochoro ambavyo magavana hawawezi kuenda. Magavana wataingia hivyo vichochoro wakati wa kutafuta kura tu lakini Wabunge wataingia huko wakati wa kutafuta kura na wakati watakapopata ushindi. Kwa hivyo, Mhe. Esther Passaris, wazo lako ni nzuri lakini si wazo la kufikiriwa katika Kenya ya sasa na Afrika ya sasa. Ni wazo la kufikiriwa wakati ambapo ufisadi katika nchi hii utapigwa vita vile ambavyo inatakikana. Siku ambayo tutamaliza ufisadi ndiyo siku ambayo labda ataleta wazo kama hilo. Ukisema tuweke pesa kwenye mfuko mmoja, tumepatia mtu mmoja nguvu ya kusema ni nani atapewa hizo pesa. Leo niko katika serikali, kesho ninaweza kuwa upinzani. Nikiwa upinzani niende kuomba pesa ya watoto wangu kule Nyali, wataniangalia na jicho la upinzani. Kama hanipendi, ataniangalia na jicho la kuonyesha mimi sina haja na wewe. Itabidi nijipange. Kwa hivyo, wazo la Mhe. Passaris ni nzuri, lakini si la karne hii. Ni wazo ambalo litafanyika katika siku za usoni wakati tutakomboa nchi hii kutoka minyororo ya ufisadi na kuhakikisha kila pesa inafikia mwananchi. Shukrani sana, Mhe. Spika wa Muda."
}