GET /api/v0.1/hansard/entries/1476792/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1476792,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476792/?format=api",
"text_counter": 114,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii nitoe maoni yangu kuhusu ripoti iliyowekwa hapa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kawi katika Seneti. Mimi na Kenya nzima tulishuhudia wakati Mhe. Chirchir alipokuwa Waziri wa Kawi, Kenya nzima ilikosa umeme usiku kucha. Jambo hili lilijirudia wakati Waziri mpya Mhe. Opiyo Wandayi alipochaguliwa. Punde tu alipoenda kufanya sherehe, tena Kenya nzima ikawa katika hali ya giza. Nyakati hizi zote mbili, Kenya ambayo iko miongoni mwa nchi zilizo na uchumi mkubwa katika Bara la Afrika ilipata aibu. Tumeelezewa kuna shida ya instability ya kubeba kawi kutoka sehemu moja hadi nyingine. Tumeambiwa KETRACO wanapata shida kwa sababu ya instability ya ile system . Juzi tumepata habari kutoka kwa vyombo vya habari na kwingineko kwamba, kuna watu wanaotaka kuekeza katika idara ya kawi na kikundi hiki ni cha watu wa Bw. Adani. Tungependa sana Kamati ya Kawi wawaite hawa watu kuhusu uekezaji wa pesa zao na za wananchi wa Kenya katika idara hii ya kawi. Tunataka kujua kama kuna ukweli kuhusu maneno ya KETRACO. Na kama ni ukweli, je, mipango hii iko wazi? Hatutaki kukaa kungojea halafu tuje kuambiwa baadaye kama haya yanayofanyika kwa upande wa uwanja wa ndege Tunataka Kamati hii ya Kawi ya Seneti watafute ukweli. Wamuite Waziri wa Kawi, Katibu wa Kudumu, Kampuni ya KETRACO waelezee Wakenya kama kuna ukweli dhidi ya madai haya ya kwamba kuna uwezekano wa kuleta pesa ili stability ipatikane katika usambazaji wa kawi nchini Kenya. Jambo la pili na mwisho, nimefurahi sana na ninampongeza Sen. Hamida kwa kuyashughulikia sana mambo ya afya ya akili. Ningependa kamati hii inapoangalia suala alilolileta hapa kwa Seneti, ikiwezekana, tunataka kujua kungewekwa pesa ama uekezaji katika kila kaunti ya Kenya kwa ajili ya wafanyikazi wa Serikali wanaopata shida ya kimawazo hasa wale wanaofanya kazi za usalama. Ingekuwa jambo la maana kamati pia iangalie kama kaunti zote tungekuwa na vituo ambavyo wafanyikazi wa Serikali haswa wa idara ya usalama wanaweza kwenda na kupata usaidizi. Tumepata shida nyingi na habari za watu wetu wanaofanya kazi kwa vitengo vya usalama. Unasikia mfanyikazi aliwacha kazi kwa sababu ya yale mambo mazito aliyoyaona kule alikoenda kuhudumu. Watoto wanaumia baada ya mfanyikazi kurudi kwenda kazi za mjengo kwa sababu hawezi rudi huko tena. Tunapoteza watu wengi ambao wangeendelea kutusaidia kwa vitengo vya usalama. Tunaomba kamati ya Seneti itakapokuwa inaangalia mambo hayo, iangalie pia uwezekano wa kutoa mapendekezo kwamba kila kaunti tuwe na mahali ambapo wafanyikazi wa Serikali wanaweza kwenda kupata usaidizi kwa mambo ya afya ya akili. Asante sana. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}