GET /api/v0.1/hansard/entries/1476826/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1476826,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476826/?format=api",
"text_counter": 148,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kwa hivyo, sisi tukiwa Maseneta, tungeungana pamoja tupinge yale ambayo Serikali kuu na pesa ile ambayo MPs wametupatia; tuipinge zile pesa, shilingi bilioni 380, kwa sababu ni kidogo. Wale MPs ambao wametupatia pesa hizi, wengi wao wamekuwa wakisema kuwa magavana hawafanyi kazi. Ningetaka kuwaambia MPs wote katika Kenya nzima kuwa, kuangalia mambo ya kazi katika kaunti sio wajibu wa MP, ni jukumu la sisi, Maseneta. Hata tunapotetea kaunti katika mambo ya pesa, wamekuwa na shida hata ya kulipa mishahara. Wafanyi kazi wa kaunti nyingi ikiwemo Kaunti ya Embu, huwa wanakaa hata miezi mitatu kabla ya kulipwa mishahara yao. Kama saa hivi, kutoka mwezi wa saba, mwezi wa nane na sasa mwezi wa tisa, Wizara inayohusika na fedha haijatuma pesa kwa kaunti zetu. Magavana wanaumia sana. Ningeomba Serikali kuu iweze kuwapatia magavana pesa vile inafaa. Tukiangalia katika constituencies, unakuta MP mmoja amepatiwa pesa shilingi milioni 150. Hapo hapo anaongezewa shilingi milioni 60 za miradi ya barabara. Pia tumesikia juzi kuwa wameongezewa shilingi milioni 150 za kuweka stima na Uwezo Fund. Sasa unakuta kuwa wamepatiwa pesa nyingi ilhali sisi ambao tunatetea ugatuzi na magavana wetu tunanyimwa pesa. Mimi nikiwa Seneta wa Kaunti ya Embu, ninapinga mara 100 mambo ripoti hiyo. Kaunti zipatiwe zile pesa ambazo tulipitisha ya shilingi bilioni 400 kwa sababu sisi tuko hapa kutetea mwananchi ambaye yuko mashinani. Itabidi sisi Maseneta; 67, tuamke na tutetee ugatuzi kwa sababu pesa nyingi tulizowapatia tulitarajia zifike shilingi bilioni 425. Lakini tuliwapatia shilingi bilioni 400. Ningetaka kupinga zile pesa ambazo zimetengewa gatuzi zetu. Mimi ninaunga mkono magavana wote. Hata kama wengine wako na shida kidogo lakini nawapa heko, haswa magavana wa kike. Kuna Gavana wa Kaunti ya Embu na Gavana wa Kaunti ya Homa Bay. Gavana wa Homa Bay amefanya kazi nzuri sana. Ametusaidia kwa kuinua akina mama. Endelea hivyo na tunaunga mkono kazi ambayo mnaifanya. Magavana waangalie kazi ile ambayo imefanywa na Gavana wa Kaunti ya Homa Bay na Gavana wa Embu; wao wanaendelea kufanya kazi nzuri. Mimi ninapinga kabisa Mswada huu. Gatuzi zipewe pesa za kutosha. Hii pesa ya NG-CDF sina shida nayo, lakini MPs wanafaa waangalie ile kazi ambayo inafanywa mashinani. Shida ya gavana, kama ni mama amepata mtoto, anapelekwa hospitali; kama ni watoto wa ECDE, hakuna shule, na vile vile mambo ya maji. Kwa kweli pesa hizi hazitoshi. Utakuta magavana wengi wako na vita ati wafanye kazi, hawa magavana wako na shida nyingi. Mimi ningeomba kaunti ziweze kupewa pesa zile ambazo tulipitisha; shilingi bilioni 400."
}