GET /api/v0.1/hansard/entries/1476829/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1476829,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476829/?format=api",
"text_counter": 151,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chimera",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Katika Mswada huu, tumepoteza takribani shilingi bilioni 20. Tulipitisha shilingi bilioni 400 hapo awali na ninaona, katika ile orodha ya fedha inakwenda kwa kaunti zetu katika mwaka huu wa kifedha wa Serikali, ni shilingi bilioni 380. Tunaona kuna upungufu wa shilingi bilioni 20. Ni bayana kwamba magavana wetu wanapata dhiki na taabu sana katika utendakazi wao kwa sababu ya zile shida zote za fedha nchini. Miradi mbalimbali imeweza kusimama. Jana Seneta wa Kaunti ya Machakos alileta Hoja hapa Bungeni kuhusu hali halisi ya utadhimini wa miradi mbalimbali katika kaunti zetu. Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba kila siku na kila kukicha ukimwuliza gavana ni kwa nini mradi fulani umekwama, kwa mfano, kwetu, katika Kaunti ya Kwale, utapata kuwa kuna miradi ya basari ambayo tunapeana hundi ya fedha kwa wanafunzi wetu katika ule mpango wa Elimu Kwanza Initiative. Kwa sasa, mradi huo una hatihati. Wanafunzi wetu hawawezi kuenda shule kwa sababu Serikali yetu ya kaunti haina fedha. Vile vile tumepatia miradi tofauti tofauti ikiwemo kuweza kuboresha barabara zetu, kuhakikisha kwamba huduma za afya; hususan tunayo hospitali yetu ya Kaunti ya Kinango ambayo imeleta joto sana katika Kaunti ya Kwale. Utapata huduma pale zimesambaratika, huduma pale zimedorora, wagonjwa wanapata taabu, madaktari pia morali yao imekwenda chini. Sio kwamba ni mapenzi ya wale ambao wako katika uongozi katika kaunti zile, lakini ni hali hii yote ya fedha. Ninaona kwamba tunapatia serikali zetu gatuzi fedha kidogo. Niweze tu kuomba ombi kwa Serikali kuu ya kwamba ugatuzi ni kitu ambacho kinatufaidi sisi kama Wakenya. Sisi sote tulikubali kama Wakenya ya kwamba tutaleta ugatuzi ili Mkenya aweze kupata faida mara dufu pale mashinani. Siyo jambo sawa; ni jambo la kutisha ya kwamba Serikali kuu inazinyima serikali gatuzi fedha. Hata kama hamna fedha, nina imani ya kwamba uongozi wa sasa unaweza kutafuta suluhu na namna gani watakavyohakikisha kwamba serikali za ugatuzi zinapata fedha zaidi na fedha za kutosha kulipa madeni yao, na kuendeleza miradi nyanjani. Sio sawa kuwanyima fedha. Mimi nina imani ya kwamba tukipunguza haya masuala yote ya ubadirifu wa fedha, masuala yote ya kuhakikisha kwamba pesa zinaibiwa katika Serikali kuu, na kuhakikisha ya kwamba wale ambao wanachukua ushuru na wanatafuta fedha za kitaifa na umma inapatikana kwa haraka iwezekanavyo na tumeweza kuhakikisha kwamba imepatikana na magavana wamepewa fedha. Kwa sababu ikiwa tutanyamaza hapa kama Maseneta, hatupigi kelele na kila saa tunapitisha sheria ambazo zinawahujumu magavana, nafikiri sio sawa. Hawa magavana tunawalaumu lakini wanahitaji kupewa fedha za kutosha ili ugatuzi uweze kuonekana unafanya kazi kweli katika kaunti zetu. Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa fursa hii. Mimi ninaunga mkono Mswada huu lakini bado pia nina ati ati."
}