GET /api/v0.1/hansard/entries/1476902/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1476902,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476902/?format=api",
    "text_counter": 224,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii kuchangia Mswada ambao unafaa kurekebisha sheria ambayo inahusika na vyama vya ushirika, Mimi ni Seneta wa Kenya kutoka Kaunti ya Kirinyaga. Kirinyaga kuna vyama vya ushirika 14 ambavyo vinashughulika na kahawa iliyo kwenye viwanda 75. Kuna chama kimoja kikubwa cha ushirika ambacho kinashikanisha vyama vingine vidogo; chama hiki kinaitwa Kirinyaga District Cooperative Union. Chama hiki kiliundwa baada ya Kenya kupata Uhuru. Vyama vya ushirika ni muhimu. Wakulima wanaouza mazao yao kupitia vyama vya ushirika, wanaweza kusaidika kupata bei nafuu. Mswahili husema umoja ni nguvu. Kwenye ukuzaji wa mchele katika eneo la Mwea tuko na vyama vya ushirika. Chama kimoja kinaitwa Lainisha SACCO. Pia kuna Mwea Rice Growers Multipurpose Co- operative Society (MRGM) ambacho pia kinasaidia wakulima kukuza na kuuza mpunga. Tuko na vyama vya ushirika eneo la Kangai kwa sababu ya ndizi. Pia kuna vyama vya ushirika vya maziwa kama Creamer Dairy na zinginezo. Bw. Spika wa Muda, kitu ambacho kinahuzunisha ni kwamba sheria iliyoko, wale ambao wamekuwa katika vyombo vya ushirika kwa muda mrefu, wamepata matundu ya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}