GET /api/v0.1/hansard/entries/1476905/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1476905,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476905/?format=api",
"text_counter": 227,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Unapata kwamba mwenyekiti wa chama cha ushirika kama kile anaeza omba shilingi milioni 3. Katika kuomba zile pesa, mali ya dhamana ni ya wakulima. Ni vizuri tutakapoangalia marekembisho ya vyama vya ushirika tupitishe sheria ambayo itazuia viongozi hawa kukopa pesa ya wakulima bila kuhusisha zaidi ya wakulima theluthi mbili ambao ni wanachama kwenye chama cha ushirika. Jambo la pili ni kwamba vyama vingi vya ushirika vimeunda SACCO. Kaunti ya Kirinyaga bado tuko na shida. Kuna chama cha ushirika ambacho kinaitwa Rwama ambacho kilikuwa na Rwama SACCO. Tayari chama hiki kimefunga milango na pesa za wakulima. Kuna chama kingine kinachoitwa Mwireri kwenye eneo la Gichugu. Wamefunga milango na pesa zote za wakulima wakaenda nazo kwa magunia. Sheria hii ya marekembisho lazima tuashirie kwamba, mwenyekiti wa chama cha ushirika akifilisisha chama inafaa mali yake ichukuliwe na wakulima waregeshewe pesa zao. Shida ya chama cha ushirika cha Rwama imemaliza mwaka mzima bila suluhu kwa wakulima. Wakulima waliokuwa wamepata pesa kutoka kwa kahawa kupitia chama cha ushirika cha Rwama wakaweka pesa hizo katika SACCO hiyo na zikapotea. Siku ya leo wanangoja vyombo vya usalama ikiwemo DCI kumaliza kesi ili watambue pesa zao zilienda wapi. Pesa zile zilikuweko pale. Ni pesa ya matibabu, karo ya shule na ya matumizi ya nyumbani. Leo hii, bado wanahangaika. Ndio suluhisho ipatikane na wapate haki yao, hatujui itakaa miaka mingapi. Hivyo basi, ni lazima tukaze hii sheria ili hata mtu atakayekuja kuwa mwenyekiti wa chama cha ushirika asiwe hata siku moja anaingiwa na akili ya kupora mali ama pesa ya wakulima. Vilevile kuna shida kubwa kwa sababu vyama vingi vya ushirika pia vimeingiliwa na wakiritimba wakati Serikali inajaribu kupambana na mageuzi ya kuhakikisha kwamba mkulima anapata pesa yake. Kwa mfano, naomba uniruhusu nipeane mfano wa Kirinyaga. Utapata ya kwamba, katika vyama vya ushirika vya Kirinyaga vyote 14 wamekata kuwapa wakulima pesa badala yake wamejenga mtambo wa kusaga kahawa mahali panaitwa Kianga. Wale wakulima wako na kampuni ya kuuza kahawa yao moja katika soko la kahawa Nairobi. Lakini kwa sababu kuna pesa inayopewa wale mawakala wanaouza katika soko ya Nairobi iliyo asilimia mbili, wenyekiti wa vyama vya ushirika wanahongwa na asilimia moja na wanatoa kahawa ya wakulima pasipo ruhusa na The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}