GET /api/v0.1/hansard/entries/1476906/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1476906,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476906/?format=api",
    "text_counter": 228,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "kupelekea wale wakiritimba na kahawa ya wakulima inapotea. Nasema hivyo nikijua mfano mzuri ni Chama cha Ushirika cha Kibirigi. Kwa hivyo, hii sheria tuliyo nayo sasa, tukiibana ili wakora wasipate mahali pa kupenya, tutaweza kusaidia mkulima. Vile vile, kuna utepetevu. Nawashukuru wale wanaohusika na vyama vya ushirika katika Kaunti ya Kirinyaga. Kuna jamaa mzuri sana pale anayeitwa Haliam, anayefanya kazi nzuri katika vyama vya ushirika. Ndio pia naunga mkono Hoja ya Sen. Omogeni ya kugatua mambo mengi katika vyama vya ushirika ili tusaidie wakazi. Ni lazima tuhakikishe kuna wafanyikazi wa kutosha wanao shughulikia mambo na sheria inafuatwa na wale waliochaguliwa wenyekiti katika vyama vya ushirika. Wale wanaosimamia vyama vya ushirika, naona sheria imempa mamlaka Waziri wa kaunti nguvu ya kutekeleza mambo kadhaa. Yale mamlaka ni mazuri ili wafanye kazi kwa pamoja na waziri wa kilimo kuhakikisha bidhaa nyingi zinazouzwa kupitia vyama vya ushirika zinafaidi mkulima. Nikimalizia, kuna mazao mengine nchini Kenya, kwa mfano, macadamia na korosho. Ukizunguka, huwezi pata chama kimoja cha ushirika cha wale wanaouza korosho, macadamia au bixa. Hii imewapa nafasi wakiritimba wanaowafinyilia wakulima kuja kununua kwa bei duni. Juzi, macadamia ilikuwa inauzwa kwa bei duni kama chumvi. Hii yote ni kwa sababu wananchi hawajaunda vyama vya ushirika ili wauze mazao yao kwa pamoja na kufikia soko nzuri. Kwa nini? Ni kwa sababu hawajaelezewa vizuri na kukalishwa chini wasome umuhimu wa kuwa na vyama vya ushirika. Mimi kama Seneta wa Kirinyaga, nimekaa na wao chini na tukasema, tukitaka kupata bei nzuri katika mazao yetu kama macadamia, vile vyama vya ushirika vinavyotumika na wale wakulima wanaokuza kahawa, vinaweza pia kutumika kwa sababu wako na ratili, maghala ya kuweka mazao kama macadamia, wafanyikazi na usalama pia. Kwa hivyo, kama tunaelimisha wote kuwa vyuo vya ushirika ndivyo vitakuwa ili kuwaondoa katika lindi la umaskini watatufuata na tuweze kuwasaidia kuuza macadamia yao. Bw. Spika wa Muda, kati ya kaunti 47, yule mkaguzi mkubwa, yani kamishna wa vyama vya ushirika, ana ofisi Nairobi City County. Ningetaka tuwe makini kwa sababu wakati mkopo unahitajika katika vyama vya ushirika, borrowing power, yani nguvu ya kukopa inapeanwa na wakulima. Ili kuhakikisha wanaomba pesa kwa njia inayofaa, yule kamishna anafaa kukagua ili kuhakikisha kuwa kila kitu kiko sahihi. Lakini kwa muda wa miaka tano iliyoisha, wale wenyekiti wa vyama hivi walikuwa wanaomba pesa kwa halmashauri au watu binafsi ambao hawajapewa ruhusa ya kukopesha pesa. Hapa ndipo wakulima wengi wamepoteza pesa yao. Ni lazima tukaze mshipi na tujue kuwa pesa nyingi zinapitia katika vyama hivi. Tunafaa kujua nani anayefaa kupeana ruhusa ya kukopa. Saa hii mwenyekiti wa chama cha ushirika, bibi na kijana wake mmoja wanaweza kuunga mkono hoja hii kama proposers na watapata uwezo wa kukopa ata shilingi milioni 300 bila kuwahusisha wakulima. Ni lazima tuweke idadi kamili ya watu wanaofaa kupitisha hoja ili mwenyekiti apate kukopa. Asante. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}