GET /api/v0.1/hansard/entries/1477091/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1477091,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1477091/?format=api",
"text_counter": 161,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika, kwa kunipatia fulsa hii nami niweze kuzungumzia mambo ya endometriosis . Nimemsikiza Mwenyekiti wa Kamati akitoa majibu yake. Ningependa kumwambia awache mambo ya google. Kwa sababu, tulimpoteza mtoto wa kike aliyeitwa Njoki. Alienda nje ya nchi kutafuta matibabu, kwa sababu hapa Kenya hakuweza kuyapata. Kwa hivyo, hili ni jambo la dharura ambalo linatesa watoto wetu. Hata mimi wakati nilikuwa msichana mdogo nilisumbuka sana. Wengine wetu tunadharau akina mama wa kitamaduni ambao wanauza dawa za kienyeji. Mama mmoja wa kienyeji ndiye alinitibu. Kule hospitalini kulikuwa hakuna matibabu kabisa. Ninaomba wale wanaohusika katika Wizara ya Afya wapigilie hili jambo upatu. Sio mambo ya planning wakati huu tunataka action . Watoto wetu wafa na sisi akina mama tunasikia vibaya sana. Ninajua wanaume hawapati hedhi ni wanawake tu. Tuna insist leo katika Bunge hili kuwa waweze kulipigia jambo hili upatu, ili tusipoteze watoto vile tulimpoteza Njoki. Mwenyezi Mungu amulaze na wema peponi. Yule mama aliyepigania mambo haya ya"
}