GET /api/v0.1/hansard/entries/1477153/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1477153,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1477153/?format=api",
    "text_counter": 223,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika. Nimemsikiliza Mwenyekiti na ningependa kukujulisha kuwa, vile Mhe. Tandaza anavyosema, fidia ambayo watu wetu wametengewa, wengine wao hawajaipata ilhali baadhi yao tayari washapata. La kusikitisha zaidi, ile ekari elfu tatu wameshagawia watu ilhali Wabunge wa Mombasa tunapowaandikia barua ya kuwaitisha majibu, hatupewi jibu. Watu wetu hawajapewa fidia ya aina yeyote. Inapaswa kuwa asilimia sabini watakapogawiwa ile ekari elfu tatu ndiposa iwarudie watu wa Mombasa… Wamezipatiana zote na hakuna mtu wa Mombasa ama Pwani kwa ujumla amefaidika. Kamati hii inapaswa kuwashikilia hao wazee ili wapate haki yao maana wamenyanyaswa. Haiwezekani kuwa fidia imetolewa na wengine wamefaidika ilhali wengine wameachwa mpaka sasa kwa mazingizio ambayo hayaeleweki. Sisi tulipewa barua iliyowataka wale watu elfu moja, mia sita na kumi na nne waendee fidia yao. Inakuwaje leo wengine wamekosa ilhali wengine wamepewa? Jambo hili lazima liangaliwe kwa kina."
}