GET /api/v0.1/hansard/entries/1477354/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1477354,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1477354/?format=api",
    "text_counter": 39,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Spika. Tuko na wageni kutoka nchi mbalimbali za Bara letu la Afrika. Kuna watu kutoka nchi ambazo zinaongea Kiingereza, wengine wanaongea Kifaransa na pia Kiswahili, kwa upande wa watu wa Congo Brazzaville. Kwa ujumla, ni bora uniruhusu niongee kwa lugha ya Kiswahili. Kwanza, najiunga na wewe kuwakaribisha hawa wageni wetu kutoka Makueni kwa ndugu yangu, Sen. Maanzo, na vilevile wale kutoka Bara la Afrika wa ile Kamati ya Tabia Nchi. Tunaona Afrika sasa inakuwa kitu kimoja. Ni muhimu kuwa tunalinda mazingira yetu. Tunawaunga mkono kwa safari yao ya kutoka nchi zao za mbalimbali za Afrika. Wamekuja hapa kujionea Bunge letu la Seneti linafanya kazi namna gani. Nina matumaini ya kwamba, wakirudi nyumbani, watakuwa wameona vile Bunge la Seneti linavyofanya kazi. Karibuni sana ndugu zetu kutoka Makueni; tunawakaribisha katika Bunge la Senate. Mko na Mbunge wenu, ndugu yangu, Sen. Daniel Maanzo. Hapa, mlipiga ndipo, hamkukosea. Ikiwa itawezekana tena, basi mmrejeshe huyu Sen. Maanzo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}