GET /api/v0.1/hansard/entries/1477400/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1477400,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1477400/?format=api",
"text_counter": 85,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bw. Spika. Najiunga na wewe kumkaribisha dada na mtoto wetu kutoka Kaunti ya Kilifi na pia Mkenya. Ni Mkenya kwa sababu ametoka katika nchi yetu na amefanya mengi ya ajabu katika Kenya. Natoa kongole kubwa kwa Bi. Akida kutoka Kilifi. Wanawake wengi katika ulimwengu wanacheza kadanda lakini wengi wao hawatafika kile kiwango chake. Huyu dada - Ms. Esse Akida - amefanya bidii, akatia juhudi na kushughulika sana kufanya mazoezi na kuangalia taaluma mbalimbali za wale walio mbele yake ili kujifunza na hatimaye akafika kile kiwango cha kucheza kadanda ya kulipwa katika nyadhifa za juu za nchi za ng’ambo. Bw. Spika nampa kongole vilevile kwa sababu anaichezea “Harambee Stars”---"
}