GET /api/v0.1/hansard/entries/1477403/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1477403,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1477403/?format=api",
"text_counter": 88,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Yes, Asante. Siyo rahisi kwa msichana mdogo kama huyu kutia juhudi na kufika kile kiwango. Katika harakati zake amepatana na pingamizi nyingi. Tumesoma katika vitabu kuwa ikiwa wewe ni mchezaji pengine una watu wanaokufunza au kukusaidia. Kumekuwa na chnagamoto nyingi katika maisha yake lakini ameweza kuzivuka na ameandika kitabu. Katika kitabu chake anasema kuwa ni kama alikuwa amefungwa minyororo lakini sasa amejifungua na anaweza kwenda kwa sababu yale mawingu hayatakuwa ya mwisho. Huenda akayavuka pia na kuingia katika ulimwengu mwingine wa uchezaji kadanda. Sisi tunamtakia kila la heri. Nawaomba Masenata na dada zangu hapa katika Bunge hususan dada yangu pale ambaye anajihusisha na mambo ya akina mama. Kama itawezekana wanunue kitabu hicho ili kuwajua wasichana wetu nchini na nyadhifa mbalimbali na mateso wanayopata lakini wanafanya juhudi mpaka mwisho wanafaulu. Nawauliza dada na ndugu zangu kama Sen. Cherarkey- kijana mdogo - awe katika mstari wa mbele kununua kitabu hicho. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}