GET /api/v0.1/hansard/entries/1477420/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1477420,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1477420/?format=api",
"text_counter": 105,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii kujiunga nawe kumpa kongole dada yetu, Esse, kwa kazi nzuri anayofanya. Esse ni mmoja wa wale wanamichezo wetu ambao wamebobea kucheza katika ligi za kimataifa. Mwingine ni Bi. Mwanahalima Adam Jereko ambaye anacheza kule Marekani sasa hivi. Bi. Mwanahalima ni msichana aliyelelewa Likoni, mjini Mombasa. Kwa hivyo, Sen. Aaron Cheruiyot, usifikiri kwamba haya mambo yanatokea Kilifi peke yake. Mombasa pia kuna mambo kama hayo. Bw. Spika, nilipata fursa ya kutembea mpaka kule Bamba katika Uwanja wa Moving the Goalposts (MTG). Nafikiri ni mradi mzuri ambao kaunti zetu zote zinafaa kuiga. Kuna Mswada wa Sen. Sifuna kuhusiana na kutengwa kwa asilimia fulani ya bajeti za kaunti kusaidia kukuza michezo. Hiyo ni njia itakayosaidia pakubwa kutoa wanatalanta wengi kama Esse ambao hawajapata fursa kama hii ili wasonge mbele katika talanta zao kama vile michezo. Kwa kumalizia, ni masikitizo kwamba wakati wasichana wetu wanabobea michezoni, wanakwenda nchi nyingine kucheza ligi kubwa kubwa huko. Hapa Kenya, hatuna uwanja unaoweza kuandaa mechi unaokubaliwa na FIFA. Ni aibu kubwa kwamba tunakwenda kuchezea mechi zetu Uganda. Timu ya nyumbani inachezea Uganda kwa vile hatuna uwanja wa kimataifa wa kuandaa mechi zinazoratibiwa na FIFA. Ni changamoto ambayo imetolewa na dada yetu, Esse, ambaye yuko hapa leo. Kwa hivyo, sisi kama Maseneta ni lazima tuangalie njia itakayosaidia kukuza michezo nchini mwetu."
}