GET /api/v0.1/hansard/entries/1477759/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1477759,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1477759/?format=api",
    "text_counter": 104,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Ningependa kuchangia Kauli ya mashamba ya ADC ambayo yamo humu nchini. Kuna wafanyakazi ambao wanafanya kazi kwenye mashamba haya. Wanaishi kwenye madongo poromoka. Hawalipwi kwa wakati unaostahili. Watoto hawaendi shule, ilhali wakurugenzi na wasimamizi wa mashamba haya wanaishi Maisha ya starehe bila kuwahurumia wafanyikazi hawa. Kauli hii inaenda sambamba na Kauli ya unyakuzi wa mashamba. Katika Jumba hili niliuliza maswali kuhusiana na idadi ya mashamba ya umma katika Kaunti ya Bungoma. Takriban miezi minne iliyopita majibu bado hayajaletwa. Hii ni ishara tosha kwamba sisi kama Bunge la Seneti tusipochunga mashamba katika kaunti zetu, zitanyakuliwa. Wakati wa ujenzi wa miundo mbinu na msingi katika kaunti zetu tutakosa sehemu za kuboresha maisha ya watu wa kaunti tunazotoko. Ni lazima tujimwae, tujizoezoe, ili kuhakikisha kwamba tunalinda mashamba ya kaunti ili vizazi vijavyo viweze kunufaika na mashamba haya."
}