GET /api/v0.1/hansard/entries/1477873/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1477873,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1477873/?format=api",
    "text_counter": 218,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika wa Muda, sikubaliani na Sen. Chute kutoka Kaunti ya Marsabit. Amezoea vibaya sana. Kitu chochote ambacho hajahusishwa, Seneti haiwezi kuendelea vizuri. Sen. Chute, wewe ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uwiano na Utangamano na unafanya kazi nzuri, lakini kitu chochote kinachokuja kwa Bunge hili na hujahusishwa, unaleta shida. Tuko kaunti 47. Huyo mtu unayemtaka ni rafiki yako na ametemwa. Umesema kwamba utakuja kumtetea. Bw. Spika wa Muda, nataka kumueleza Sen. Chute kwamba mambo mengine ni lazima aachie watu wengine. Siyo kila kitu ahusishwe. Anataka ahusishwe kwa kila kitu. Ukiangalia upande wa nyumba, mafuta na kila kitu, ni Sen. Chute anahusishwa. Kenya sio Marsabit. Ni lazima ujue kwamba tuko Maseneta 67 na kaunti 47. Kwa hivyo, haiwezekani Sen. Chute ahusishwe kwa kila kitu."
}