GET /api/v0.1/hansard/entries/1477884/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1477884,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1477884/?format=api",
"text_counter": 229,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika wa Muda, sina tashwishi yoyote kwamba hii ni Bunge ya wazee yaani ‘ Upper’ House . Nimekasirika niliposikia Sen. Chute akiongea kuhusu Kaunti ya Marsabit ilhali tuko na kaunti 47 na Maseneta 67. Sisi sote huwa tunaleta amani Kenya hii. Tunajua kwamba Sen. Chute ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uwiano na Utangamano na maneno aliyoongea hayakunifurahisha. Seneta wa Kaunti ya Mombasa, wewe ni rafiki yangu. Sina shida yoyote lakini matamshi ya Sen. Chute ndiyo yamefanya roho yangu iende juu. Mimi ni rafiki wa kila mtu na kila kaunti. Sikuwa na shida yoyote. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}