GET /api/v0.1/hansard/entries/1477945/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1477945,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1477945/?format=api",
"text_counter": 290,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kazi mapema katika hii kipindi ya Serikali ya muungano, angelainisha mambo mengi iliyoharibika. Alipotoka sekta ya kawi, ndipo tukaskia kwamba KPLC ilinunua transformer ambazo hazifanyi kazi vizuri kwa sababu ya ukosefu wa competition katika kampuni ya kusambaza umeme, isipokuwa KPLC. Labda angetupa ujuzi wa kuwa na competition ya umeme. Bw. Spika wa Muda, kuna mambo mengi ambayo tunataka yafanyike kwenye sekta ya kilimo. Katika Kaunti ya Embu, kuna miraa/muguka . Angekuwa amechunguza kuhusu dawa itakayosaidia kukuza miraa bora ili watu wasiwe wagonjwa. Naunga mkono kuteuliwa kwa Bw. David Kemei kwa sababu angekuwa amechunguza idara nyingi na kutenda kazi. Atahakikisha kuna competition katika kila department ili kazi ifanywe vile inapaswa kufanywa. Ana miaka mingi huko mbele na ataweza kutupa ujuzi na kuwatafutia vijana wetu kazi kwenye kila kona kulingana na ujuzi wao. Naunga mkono Serikali ya muungano na ningeomba Maseneta wote wamuunge mkono Bw. David Kemei ili tuone akakavyotufanyia kazi. Napinga wanaosimama kusema kwamba wangeleta majina matatu au mawili. Kazi yetu ni kuunga mkono lile jina moja tu ya David Kemei, ambayo tumeletewa hapa. Hiyo ndio kazi yetu ya kuchambua stakabadhi zote ya David na tumpitishe ili afanye kazi. Ninapinga wale watu ambao wanasimama kusema huyu ni wa kaunti hii na ile. Wengine wanasema ni wa mlima. Napinga Maseneta ambao wanasimama kuongea mambo ambayo hayaeleweki katika Seneti hii. Kwa hivyo, ninaunga mkono. Asante."
}