GET /api/v0.1/hansard/entries/1478477/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1478477,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1478477/?format=api",
    "text_counter": 127,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika. Swali langu linatoa dosari kidogo kwa yale umesema, ila naomba uniruhusu kuuliza Bw. Waziri kwa yale ataweza kujibu. Kwanza, nashukuru Waziri wa Hazina na Fedha kwa sababu aliteuliwa ili asaidie katika mambo ya fedha kwenye hii Serikali ya muungano. Alionekana kuwa ataweza kufanya kazi hiyo. Kwa hivyo, nampongeza. Bw. Waziri, katika Kaunti ya Embu, mambo ya fedha huchelewa sana. Unafahamu kwamba tulikubali kuwa katika kipindi hiki cha Serikali ya muungano, pesa iwe ikitumwa kwa kaunti kila mwezi. Mwezi wa saba, wa nane na wa tisa, Kaunti ya Embu haikupata pesa na kumekuwa na malalamishi ya pending bills na wage bill. Shida kubwa sana ni kwenye sekta ya ukulima na pesa za kununua dawa. Naomba ikiwa una uwezo wa kujibu ijapokuwa Spika amesema haiwezikuwa swali lisilofanana na zile uliloulizwa, najua una njia ya kujibu swali hilo. Huenda ikawa sio Embu pekee, tuna kaunti 47. Asante."
}