GET /api/v0.1/hansard/entries/1478487/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1478487,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1478487/?format=api",
"text_counter": 137,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Mimi najiunga na Maseneta wenzangu kumkaribisha Waziri, Mhe. John Mbadi katika Bunge la Seneti na pia kumpa kongole kwa kuchaguliwa kuwa Waziri katika Serikali. Dukuduku langu ni kuhusiana na swala la ucheleweshaji wa fedha kwa kaunti zetu kwa sababu baada ya kuondolewa kwa Mswada wa Fedha wa Mwaka 2024/2025, kumekuwa na sintofahamu ni vipi watapeleka pesa katika kaunti zetu. Ninakumbuka mwaka 2019 tulikuwa katika hali hii, lakini kwa wakati ule Serikali iliyekuwa mamlakani ilipeleka asili mia fulani ya fedha kwa kaunti zetu. Ninaomba Waziri atueleze, ni sababu gani kaunti haziwezi kupewa asili mia fulani mpaka asili mia hamsini ya zile fedha ambazo walipewa mwaka jana ili waweze kutumia kukithi mahitaji yao tunapongojea sheria mpya iwe tayari."
}