GET /api/v0.1/hansard/entries/1478838/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1478838,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1478838/?format=api",
"text_counter": 173,
"type": "speech",
"speaker_name": "Tigania East, NOPEU",
"speaker_title": "Hon. Mpuru Aburi",
"speaker": null,
"content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Yangu ni machache. Kuwa na scientific museum katika nchi yetu ya Kenya ni jambo la maana. Hii ni kwa sababu hapo awali, kulikuwa na mashine ya kutengeneza unga kabla zile mashine za Lister zije. Tulikuwa na zile ambazo zilikuwa zinazungushwa na maji. Kulikuwa na mawe mawili ambayo yalizungushwa na maji kutoa unga wa ugali. Lakini ukiwaelezea watoto wa kisasa kwamba kulikuwa na mashine kama hiyo, hawawezi kuelewa maana nasi tulisahau. Zamani mtu angekatwa na panga, kulikuwa na mti aina fulani uliotumika kama dawa. Huo mti ungekatwa na maji yake yakaguzishwa kwenye mkono uliojeruhiwa na ungeshikana. Vijana wetu wa kisasa wakiulizwa hayo mambo, hawawezi wakajua. Ndiposa, lazima tuwe na makavazi ya kisayansi."
}