GET /api/v0.1/hansard/entries/1479240/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1479240,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1479240/?format=api",
    "text_counter": 391,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": "kushikana pamoja na Wajumbe wenzangu katika kuunga mkono uteuzi wa Bwana David Kemei katika Mamlaka ya Ushindani ya Kenya. Vile vile, niko na sababu ambazo zinanifanya niunge mkono Hoja hii. Watu wengi wameongea kuhusu utendakazi wa Bwana David Kemei. Wamesema kuwa ni mtu ambaye atasaidia kuhakikisha kuwa halmashauri hii imenawiri. Tumemsikia Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi, ndugu Kimani Ichung’wah, akizungumzia juu ya hali ilivyo katika KenyaPower . Ni muhimu nami nimuunge mkono na kusema kuwa ni muhimu mwananchi aweze kujichagulia. Lakini hali ilivyo sasa, mwananchi hana budi. Lazima atumiwe nguvu za umeme za Kenya Power . Vile vile, nataka kumwambia Bwana David Kemei kuwa kazi yake ni ngumu sana. Lazima ajitolee na lazima Serikali impe nguvu za kuhakikisha kuwa ameimarisha ushindani baina ya mabwenyenye ambao watakuwa wakitaka kuzuia kazi yake ili waweze kumonopolise biashara. Katika uwekezaji wa nafaka, yaani grain handling, kuna makampuni ambayo yanataka kushindana na makampuni mengine kule Mombasa, ili yafanye biashara ile. Lakini makampuni hayo yanawekewa vikwazo vingi visivyowaruhusu katika uwanja wa ushindani, ili yafanye biashara ile. Kijana mmoja ambaye ni mkurugenzi mchanga sana pale anayeitwa Mohamed aling’ang’ana na mambo ya documentation na mengine mengi, ili ashindane na wale mabwenyenye wengine. Hatuwezi kuinuka ikiwa tutaacha wale mabwenyenye peke yao wenye nguvu wafanye biashara. Kwa hivyo, ni muhimu kwa Bwana David Kemei kusikiliza yale maneno ambayo tutamweleza atakapoingia ofisini. Akifanya hivyo, atafungua mlango wa ushindani wa kibiashara na mambo mengine kwa watu wetu. Vile vile, leo tuna hasara. Kuna mafuta yaliyopatikana kule Turkana. Zamani, pale kwetu Mombasa, kulikuwa na refinery pale Changamwe. Hivi sasa, imefungwa na hakuna ushindani ambao unaweza kuendelea. Haya mafuta yanapopatikana, yanapelekwa nchi za nje kisha kurudi nchini yakiwa refined ndipo sisi tunauziwa. Mambo kama haya kwa Kiswahili tunasema ‘goji kiriba na kiriba goji’. Yaani, sisi tuna mafuta tuyatoe nje, tufanyiwe refining, kisha turudishiwe. Hii kampuni ya refinery lazima ifufuliwe na Serikali ili ishindane na wale Waarabu wengine katika nchi za nje. Pia, itasaidia watu wetu kupata kazi ambazo walikuwa wakifanya katika hiyo refinery . Leo, watu wengi wamefutwa kazi. Wameenda kutafuta kazi katika nchi za nje. Kuna mume wa mama yangu mdogo, anaitwa Kibwana, alikuwa mfanyakazi katika refinery . Kwa experience yake, baada ya refinery kufungwa, sasa anafanya kazi Qatar, ambayo ni nchi ya nje. Wanasaidia watu wengine na hali ni radi ikifunguliwa wataleta ushindani na watu wetu kufanya kazi hapa. Mhe. Spika wa Muda, nashukuru sana. Pia nampongeza Bwana David Kemei. Ahsante sana."
}