GET /api/v0.1/hansard/entries/1479861/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1479861,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1479861/?format=api",
"text_counter": 34,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Ahsante, Mhe. Spika. Nampongeza Mheshimiwa kwa kuleta swala hili la mihadarati hapa Bungeni. Kusema kweli, hili swala linatuathiri sana. Kabla sijaendelea kuchangia, nataka Mheshimiwa achukue tahadhari. Mimi nilitaja majina ya wanaohusika na uuzaji wa madawa ya kulevya katika eneo bunge langu na hiyo ilikuwa mwanzo wa maisha yangu kubadilika. Ilikuwa katika Bunge la 12 ambapo nilikasirika na nikataja majina ya wahalifu hao. Baada ya kutaja majina yao, maisha yangu yalibadilika na ilinibidi niwe nikitembea na askari kila mahali. Niliongezewa askari waliokuwa wakinilinda. Nashukuru Bunge hili kwa sababu lilinisaidia sana. Hii shida ipo na ukiizungumzia, wewe ndio unaonekana mbaya. Wale wanaouza mihadarati si wabaya. Wewe unayezungumzia swala hilo kama Mbunge ndio unaonekana mbaya. Kuna siku nilienda kwa mkutano na nikazungumzia swala hilo. Mtu alikuja na kunishika na akaniambia nisizungumzie maneno hayo. Nikiyazungumzia nitawaletea shida. Wanaouza mihadarati wana power zaidi kushinda hata Mbunge. Unakatazwa hata usizungumzie swala hilo. Wakati nilipokuwa naomba kura, drug dealers wa Lamu West wote walikuja Lamu East kunipinga ili nisipate kura. Lakini Mwenyezi Mungu akawa nami na nikapata ushindi. Tatizo hili ni kubwa sana Lamu East. Percentage ya youths wetu wanaotumia madawa ya kulevya inaongezeka. Nimesahau nambari hizo lakini Kenya Red Cross wako nazo. Nimeshangazwa na jinsi asilimia hiyo inaongezeka. Watoto wameathirika sana. Wako"
}