GET /api/v0.1/hansard/entries/1479866/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1479866,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1479866/?format=api",
"text_counter": 39,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "ndiyo imeathirika zaidi. Hapo awali, mihadarati ilikuwa janga la eneo la Coast pekee yake. Lakini sasa, cocaine imekuwa janga la Kenya nzima. Kule Lamu East, shida si cocaine pekee yake. Kuna tembe zinazoitwa karambela . Nimezizungumzia mpaka katika security meetings. Nimeambiwa nizilete ili wazione kwa sababu hawazijui. Mwishowe, waliniambia walizipata. Karambela inauzwa kwa Ksh20. Mtu akizikula, anageuka na kuwa kama wild animal . Anaweza kufanya chochote. Zinauzwa na hakuna hatua inayochukuliwa. Ukimtuma mtu azinunue, atapelekwa mpaka mahali zinazouzwa. Hakuna mtu ambaye hajui wanaoziuza. Shida ni kuwa hawachukui hatua yoyote kuwakomesha. Ahsante, Mhe. Spika."
}