GET /api/v0.1/hansard/entries/1479886/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1479886,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1479886/?format=api",
"text_counter": 59,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaloleni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Paul Katana",
"speaker": null,
"content": " Ahsante, Mhe. Spika. Swala la mihadarati ni swala nyeti sana. Zamani, madawa ya kulevya yalikuwa yanapatikana mijini. Kufikia sasa, yameingia mpaka mashinani. Wanaoumia zaidi ni watoto wa shule ambao siku hizi wameanza kujiua kwa sababu wakila madawa ya kulevya, kufikiria kwao kunakuwa duni. Tujiulize swali moja. Huku Kenya, hatuna shamba la cocaine wala heroin . Hayo madawa yote ya kulevya yanatoka nje ya nchi yetu. Ni wapi ambapo kuna ulegevu ambao unaruhusu madawa ya kulevya kuingia nchini? Kama vile ndugu yangu amesema, kuna baadhi ya vitengo vya usalama ambavyo vinajua ni akina nani ambao wanaleta na kuuza mihadarati. Lakini hao watu hawawezi kushikwa kwa sababu wanalindwa na wanalipa baadhi ya polisi wetu ili waweze kuwalinda waendelee na biashara yao haramu. Ni wakati mwafaka kama taifa, bila kumulaumu mtu yeyote, kuharamisha mihadarati nchini kwa sababu inahatarisha usalama wa kitaifa. Ahsante, Mhe. Spika, kwa kunipatia nafasi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}