GET /api/v0.1/hansard/entries/1479980/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1479980,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1479980/?format=api",
    "text_counter": 153,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana Mhe. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii nami niweze kumshukuru mzee mwenga kwa kuweza kuwalea hawa vijana wawili. Leo hii ni Wabunge ambao tuna wa sherehekea ndani mwa hili Bunge. Imenikumbusha mzee marehemu Mhe. Yusuf Haji, ambaye alinisomesha na ndio maana munaona jambo lolote likija hapa la Noordin Haji, ni lazima nimpigie upeto kwa sababu yeye ni ndugu yangu. Sisi ambao tumetoka katika familia maskini, tukasomeshwa na kunyanyuliwa na wale ambao wanatuonea huruma, siku zote sisi huwa na huruma na ndio maana huwa tunarudi kwenye jamii na tunazidisha upendo kwa wale ambao hawawezi kujimudu katika maishi na sisi pia tuweze kuwasaidia. Vile nimepata fursa, ningependa kwanza kumpongeza Waziri wa Mazingara kwa kuja hapa bungen. Ahsante sana, tunakushukuru. Umesema kwamba mambo ya maji taka na vinginevyo ni mambo ya kaunti. Lakini pia tukiangalia kaunti ya Mombasa, pale Tudor, maji taka yamekuwa yakiingia ndani ya Bahari kwa miaka mingi sana, na watoto wanaoishi katika sehemu za vitongoji duni wanaenda kuogelea kule. Hii ni kwa sababu watu wamejenga nyumba bila ya kuangalia maji taka yatakwenda vapi. Wakishamaliza kujenga, wanaelekeza mabomba ya maji taka kwenye bahari. Nakuomba, kama unaweza, ulifuatilie jambo hili. Umesema hayo masuala ya serikali za kaunti, lakini nakusihi manaake wakati mwingine barua ikitoka kwa Waziri, pengine jambo linaweza kufuatiliwa na kufanywa kwa wepesi. Mhe. Waziri, umesema tunapanda miti ambayo pia itatupatia matunda. Mimi, kama mama Mombasa County, nimezunguka na nikaangalia miti. Minazi imekuwa michache sana ndani ya pwani. Nakuomba, kama mama Mombasa County, utuletee miche ya minazi na miembe ili tuweze kupanda tupate kuvuna matunda kama chakula na pia iweze kutuletea mvua. Ahsante sana."
}