GET /api/v0.1/hansard/entries/1480146/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1480146,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1480146/?format=api",
    "text_counter": 319,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ya kumuuliza Waziri maswali. Mwanzo, ninachukua nafasi hii kumpongeza Waziri. Kusema kweli, tumekukosa hapa Bungeni. Tulikuwa tumezoea kuisikia sauti yako sana. Tumekumbuka sauti yako wakati ulipokuja. Nilipopata nafasi hii, nilijiuliza ni jinsi gani huyu mfugaji wa mifugo atawiana na mazingira. Lakini nimeona umekuwa bingwa wa kuhifadhi mazingira, kiasi kwamba ukiyazungumzia, maneno yako yanatoka rohoni kabisa. Kushughulikia mazingira kumekufanya uyapende. Ninaona ushaingiliana huko vizuri. Pongezi kwa hayo. Niliuliza swali kuhusu eneo la Siu. Kampuni ya Zarara ilijaribu kuchimba gesi lakini gesi hiyo haikupatikana. Hawakufunga kile kisima walichokichimba vizuri kwa hivyo kuna moshi unaotoka pale ambao umewaogopesha watu, na maeneo hayo yamebadilika rangi. Yule mtu aliyekuwa akilinda kisima hicho alifariki kwa hivyo watu wameanza kuwa na wasiwasi. Nilipouliza swali hilo Bungeni, nilijibiwa kwa barua. Mabadiliko ya Serikali yalikuwa yametokea wakati huo kwa hivyo swali langu halikujibiwa vizuri. Niliuliza nijibiwe tena kwa sababu sikuwa nimetosheka lakini yale mambo yalipotelea hapo. Leo ninawaomba mhakikishe kuwa swali langu limejibiwa maanake mambo yaliyozungumziwa hayakuwa sawa na hali ilivyo kule mashinani. Bwana Waziri, nimekusikia ukisema kuwa swala la takataka linashughulikiwa kwenye kaunti. Ni kweli kuwa linashughulikiwa na kaunti lakini sina uwezo wa kuenda kwenye kaunti kuulizia. Nipo kwenye Bunge kwa hivyo, nitakuuliza wewe. Tumepanda miti katika asilimia 42 ya Kaunti ya Lamu. Sisi ni nambari ya pili Kenya nzima kwa kupanda miti. Eneo Bunge langu la Lamu Mashariki lina vijiji 23. Kuna upande wa msitu na ule wa Bahari. Watu wangu wanang’ang’ana kuhifadhi msitu lakini hakuna mpangilio wowote wala ishara yoyote kutoka kwa Serikali ya kitaifa na serikali ya kaunti kuonyesha kuwa kuna kitu kinachofanywa. Mnatupatia morale vipi? Bwana Waziri, nilikusikia ukitaja upande wa bahari. Ninakuomba uingize upande huo katika fikra zako kwa sababu hakuna Waziri yeyote anayekuja hapa Bungeni anayetaja Lamu Mashariki. Ninaomba utufikirie maanake kule kwetu, hakuna mahali ambapo birika la kuweka takataka limetengenezwa. Ninaomba utufikirie maana kule kwetu hakuna hata pahali pametengenezwa pa kuweka takataka. Zote zinawekwa kwa bahari. Kwa hivyo, ninataka ufikirie jambo hili. Kama kuna mpangilio wowote, nasi utufanyie. Ama kama haukuwa umefanya, uniambie ni upi. Niko mashinani na sijaona pahali."
}