GET /api/v0.1/hansard/entries/1480613/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1480613,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1480613/?format=api",
    "text_counter": 268,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika. Nasimama hapa kuunga mkono Hoja hii ya kumng’atua mamlakani Naibu wa Rais, Bw. Rigathi Gachagua. Naunga mkono kwa sababu Katiba yetu, katika Kifungu 159, imetupatia sababu mwafaka za kuweza kumng’atua Naibu wa Rais. Sababu ya kwanza imezungumzia kukiuka Katiba. Mhe. Rigathi Gachagua amekiuka Katiba haswa nikiangalia Kifungu cha 10 ambacho kinazungumzia maadili ya Kitaifa, ikiwemo umoja, demokrasia, na usawa. Mara nyingi sana amezungumzia mambo ya nchi yetu kwamba ni kama kampuni na ni ya washikadau. Hawa ni wale watu ambao walipigia serikali ya Kenya Kwanza kura. Hivyo basi, amekiuka maadili katika Kifungu cha 10. Ni kwa sababu tunajua Wakenya wote wanalipa ushuru na wana haki sawa kila mmoja: wale waliopigia serikali kura na wale ambao walikuwa upande mwingine. Kwa sababu ni demokrasia, unaweza kuwa upande wa serikali ama upande wa upinzani."
}