GET /api/v0.1/hansard/entries/1480614/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1480614,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1480614/?format=api",
    "text_counter": 269,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": "Vile vile, Kifungu 147 cha Katiba kinasema kwamba yeye atakuwa msaidizi mkuu wa Rais katika serikali na naibu katika zile kazi ambazo Rais anazifanya. Lakini, je, vitendo vyake vimeonyesha maneno hayo? Vimeonyesha kwamba yeye si msaidizi. Wakati ule wa maandamano ya Gen Z Rais alitoa hotuba hapa Nairobi ya mwelekeo wa taifa kuhusu jambo lile. Yeye alikuwa Mombasa akitoa hotuba ambayo ilikuwa inazungumza tofauti na ile ya Rais. Hapo pia akatia fitina katika taasisi zetu za kiserikali na kumlaumu Bw. Noordin Haji. Inaonyesha kwamba yeye ni kama anachukua nafasi ile ya Rais wala si msaidizi. Vile vile, tumeona Naibu Rais amekiuka Katiba na kuwa na utovu wa nidhamu wa hali ya juu. Kwa Kiingereza tunasema gross misconduct . Kwa mfano, aliita mmoja wetu, Mhe. Jematiah, malaya. Unapoita mwanamke yeyote malaya, umeita akina mama wote wa Kenya hivyo. Sisi siyo malaya: sisi ni akina mama na pia viongozi. Hatuwezi tukakubali Naibu wa Rais kutuita malaya. Vile vile, alisema hao akina mama wa Mlima Kenya ambao hawamuungi mkono ni akina mama wa Rais. Alikuwa anamaanisha nini? Mhe. Rigathi Gachagua, hauna heshima kwa akina mama wa taifa hili la Kenya."
}