GET /api/v0.1/hansard/entries/1480619/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1480619,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1480619/?format=api",
"text_counter": 274,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": " Hii pombe haramu, iko Mlima peke yake ama pia iko kule Magharibi, Nyanza, na Nairobi? Tumwulize, zile milioni ametumia kwa hiyo kazi, zimetupatia natija gani? Zimekuwa na faida gani isipokuwa kunyakua ardhi na kuandika jina la mke wake, ati atatengeneza sehemu za kunasua vijana katika jambo hilo? Jambo lingine ni kashfa ya KEMSA ambayo imezungumziwa vizuri sana. Aliwezesha watoto wake na makampuni yake kuiba pesa zile katika kashfa hiyo. Hatuwezi kuwa na Naibu wa Rais ambaye juzi tu mali yake ilikuwa Ksh800 milioni na hivi sasa mali yake ni Ksh5.2 bilioni. Pesa hizi amezipata wapi kwa muda mfupi?"
}