GET /api/v0.1/hansard/entries/1480623/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1480623,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1480623/?format=api",
    "text_counter": 278,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": " Tunajua sheria inazungumzia njia ya kurithi mali wakati mume amekufa. Bibi na watoto wanarithi mali. Itakuwaje wewe uchukuwe huo urithi wote, mpaka hoteli? Ati ulisema ndugu yako alikupa mali. Jamani, wewe kama Naibu wa Rais, muogope Mwenyezi Mungu. Pia, ujue kwamba hatuko hapa kwa sababu ya ukabila. Tukiangalia sheria ya Bunge ya National Cohesion and Integration, inasema yeyote atakayetumia maneno ya matusi ama kutishia ili kuleta bugudha katika makabila anatakikana ashtakiwe. Yeye amefanya makosa. Tunajua vile matamshi ya kikabila huko Rwanda yaliwatia katika vita vikali vya kikabila. Naibu wa Rais anataka kuleta vita katika taifa la Kenya. Tuliona Molo clashes na inasemekana alikuwa kwa hayo maneno."
}