GET /api/v0.1/hansard/entries/1480917/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1480917,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1480917/?format=api",
"text_counter": 150,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Kwenye Bunge letu la Seneti iliwakilishwa na Sen. Cheruiyot ambaye ni Kiongozi wa Wengi na vile vile Sen. Omogeni ambaye aliwakilisha upande wa wachache. Ni muhimu kwamba sheria zetu za uchaguzi zipigwe msasa mara kwa mara, kwa sababu, kuna mambo yanayoibuka katika uchaguzi ambayo mengine labda hayakuweza kuangaziwa katika sheria iliyoundwa. Bi. Spika wa Muda, haifai kuwa na vituo gushi vya uchaguzi ambapo unaambiwa matokeo yanatoka katika kituo fulani ambacho hakiko kwenye orodha. Hivyo basi, Sheria hii itaharamisha matokeo ya vituo vyovyote ambavyo haviko katika orodha ya vituo vya kufanyia uchaguzi. Swala la pili linahusu wale wanaosimamia uchaguzi."
}